Habari picha: Kisiwa cha Kilwa kilitengeneza Sarafu ya Kwanza Afrika Mashariki

Historia ni mwalimu mzuri, huko katika kisiwa cha Kilwa kuna wakati ilikuwa dola inayojitawala na kusifika kwa utajiri, lakini sasa eneo hilo ni mji katika mkoa wa Lindi ulioko kusini mwa Tanzania.

Magofu ya kilwa ni maeneo machache sana duniani, eneo hili ni kielelezo tosha kuwa Afrika mashariki ilikuwa ikijihusisha sana na shughuli za kibiashara kimataifa.