Polisi Indonesia watumia nyoka kumtishia mshukiwa wa uhalifu

Chanzo cha picha, Reuters
Polisi nchini Indonesia imeomba msamaha kwa kutumia nyoka kumtishia mshukiwa wa wizi baada ya video kusambazwa katika mitandao.
Maafisa katika video hiyo wameonekana wakicheka huku wengine waliokuwa wakimhoji mshukiwa wakionekana kumtatia nyoka shingoni mwa mshukiwa huyo aliyefungwa pingu huku akipiga kelele mashariki mwa eneo la Papua.
Inaaminika mshukiwa alikuwa ameiba simu za mkononi.
Afisa mkuu wa polisi katika enee hilo, amesema haikupaswa kufanyika hivyo lakini ametetea mbinu hiyo akieleza kwamba nyoka huyo hana sumu.
"Tumechukua hatua kali dhidi ya maafisa waliohusika," Tonny Ananda Swadaya inaarifiwa alisema katika taarifa, akiongeza kwamba maafisa hao hawakumpiga mshukiwa.
Walichukua hatua kwa hiari yao kujaribu kumfanya mshukiwa akiri makosa, alisema.
Wakili anayetetea haki za binaadamu Veronica Koman ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter ulioonyesha video hiyo, akidai kuwa maafisa hivi karibuni walimtishia mwanaharakati anayetetea uhuru wa Papua kwa nyoka akiwa gerezani.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Sauti katika kando hiyo ya video inaarifiwa kusikika ikitishia kumweka nyoka huyo ndani ya mdomo wa mshukiwa na ndani ya suruali yake.
Ni kawaida kusikia ripoti za ukiukaji wa haki za binaadamu kutoka Papua, eneo ambako wanaharakati wa kutetea kujitenga kwa muda mrefu wamepigania uhuru kutoka kwa Indonesia.
Maeneo yenye utajiri wa rasilmali yanapakana na Papua New Guinea na yalijumuishwa kuwa sehemu ya Indonesia mnamo 1969.














