Uganda kuanzisha kikosi kipya cha usalama Kampala

Woman training

Chanzo cha picha, Allan Atulinda

Maelezo ya picha, Zarake Maria Goretti anasema kuwa jeshi hilo litampatia says the paramilitary force will give her job security

Serikali ya Uganda imeanzisha kikosi kipya cha usalama kukabiliana na kiwango cha juu cha uhalifu , lakini wakosoaji wake wanahofia kwamba huenda kikosi hicho kikawa mwiba dhidi ya mji huo kulingana na mwandishi wa BBC Patience Atuhaire mjini Kampala.

Zarake Maria Goretti ameketi katika nyasi baada ya kutoa sampuli yake ya damu ili kuchunguzwa kimatibabu.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 ni miongoni mwa maelfu waliojitokeza katika uwanja wa wazi , ambao hutumika kwa biashara mjini Kampala kuomba ajira ya kujiunga na kikosi hicho cha raia kinachojulikana kwa Local Defence Unit. LDU.

Takriban maafisa 6000 wa LDU kwa sasa wanafunzwa kuwasaidia maafisa wa usalama kukabiliana na uhalifu kufuatia msururu wa visa vya mauaji.

Wakosoaji wana kumbukumbu ya ni lini jeshi la raia liliwahi kuhudumu. Baadhi ya wanachama wake walishutumiwa kwa kutumia vibaya nyadhfa zao na kuwa wahalifu wao wenyewe.

'Kuzilinda familia'

Lakini bi Goretti anataka kupita vipimo vya kimatibabu na kujiunga na kikosi hicho.

Licha ya kwamba ana vyeti vya kufuzu katika usimamizi wa hoteli anataka kuorodheshwa katika ajira ya kuhudumia serikali.

"Najua nitapata kazi ya kudumu serikalini,," Bi Goretti aliambia BBC.

Allan Atulinda

Chanzo cha picha, Allan Atulinda

Maelezo ya picha, Watakaofuzu watahudumu katika maeneo wanayotoka

Kwa upande mwengine Abue George William, mwenye umri wa miaka 32 amekuwa na ari ya kutaka kulinda taifa.

''Nitahakikisha kuwa kila familia iko salama , hakuna wezi mitaani na kila mtu ana haki ya kutembea hata usiku wa maanane'', alisema.

Maafisa wa kikosi hicho kipya wanatarajiwa kutembea katika mitaa , na kutoa taarifa za ujasusi kwa maafisa wa polisi wanapokabiliana na visa vya uhalifu.

Watakaoteuliwa wameahidiwa mshahara wa ksh. 200,000 za Uganda kwa mwezi ambazo ni sawa na dola 40 za Marekani. Kuna mlolongo mrefu kama ile ya watu wanaotafuta ajira.

'Sifa ya rais Museveni inatiliwa shaka'

Wanajeshi wanaongoza mkatati wa kuwaajiri maafisa hao mbali na kuwatoa wale wasio na vyeti vinavyohitajika. Wanaofuzu hulazimika kukimbia kwa kilomita nne.

Waziri wa usalama Elly Tumwiine aliambia BBC kwamba maafisa hao wa LDU wataripoti kwa jeshi na kushirikiana na maafisa wa polisi.

''Ni operesheni ya pamoja'', aliongezea.

Maafisa wa polisi mjini Kampala {archive shot)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wengine wanasema kuwa maafisa wa polisi wa Uganda ni wachache.

Walioteuliwa watafanyishwa mazoezi ya miezi minne na wataanza kazi wakiwa na silaha karibu na Kampala na maeneo mengine ya karibu.

Hatua hii inajiri kufuatia amri ya rais Museveni mnamo mwezi Septemba kuwezesha maeneo ya mijini kuwa salama.

Uungwaji mkono wa rais Museveni katika kipindi chake cha uongozi wa miongo mitatu unatokana na sifa yake ya kuwahakikishia raia usalama , hivyobasi kumaliza misukosuko ya kisiasa inayoanzia miaka ya 1960 hadi alipochukua mamlaka 1986.

Lakini tangu 2014, Kampala imeshuhudia viwango vya juu vya utovu wa usalama.

Visa vya mauaji

Takriban viongozi watano wa Kiislamu waliuawa kiholela kati ya mwezi Disemba 2014 na Oktoba 2017 mjini Kampala na viungani mwake. Mauji mengine ambayo hayakutatuliwa ni pamoja na .

  • Kiongozi wa mashtaka Joan Kagezi
  • Msemaji wa zamanai wa polisi Andrew Felix Kaweesi
  • Mwanasiasa Ibrahim Abiriga na
  • Afisa wa polisi Mohammad Kirumira, ambaye alizungumzia sana swala la ufisadi katika kikosi cha polisi.

Mwaka 2017, kulikuwa na visa vingi vya utekaji nyara na mauaji ya kiholela mbali na ongezeko la visa vya utekaji nyara na mauaji ya wanawake.

Takriban wanawake 20 waliuawa katika kipindi cha muda wa miezi minne ndani na viungano mwa mji wa Kampala na kuzua hofu na wasiwasi.

Magenge yaliojihami na silaha yalivamia baadhi ya makaazi ya mjini Kampala.

Quote box

Afisa wa zamani wa usalama ambaye hakutaka jina lake litajwe amelaumu hali mbaya ya usalama akidai inasababishwa na hali mbaya ya kiuchumi.

Vijana wamesoma na hawana kazi. Wengine wamelazimika kutumia njia mbaya za mkato ili kujikimu kimaisha.

''Magenge ya uhalifu kama vile Kifeesi yanayotekeleza operesheni zake mjini Kampala yanasababishwa na hali kama hiyo'', alisema.

Genge la Kifeesi linasemekana kuwa na makao yake makuu katika makaazi ya mabanda ya Katwe mjini Kampala na wanachama wake wana sifa mbaya ya kuvunja magari ya raia wakati wanapokwama katika trafiki na kuiwaibia.

Rais ameelezea wasiwasi wake kuhusu kushindwa kuwawinda wahalifu.

''Ni wazi kwamba idara ya ujasusi imekuwa hafifu katika kukabiliana na visa kama hivyo kama vile kisa cha mauaji ya kiongozi wa mashtaka Kagezi na wengine. Hali hiyo inatatuliwa na kuimarishwa'' , alisema rais Museveni alipotangaza uanzishaji wa LDU.

Protesters hold banners during the women's march demanding police action to stop a spate of kidnapings and murders of women in Kampala, Uganda, on June 30, 2018

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, The abduction and killing of women caused outrage

Kikosi cha polisi kina takriban maafisa 45,000 lakini waziri wa usalama anasema kuwa maafisa hao ni wachache.

Na jeshi haliwezi kusaidia kwa sababu linahusika kulinda amani nchini Somalia, kulingana na kanali wa jeshi Bonny Bamwiseki katika kituo cha kuwaajiri maafisa wa kikosi kipya mjini Kampala.

Hatuwezi kupelekewa kuweka usalama mitaani. Vijana hawa wataimarisha usalama mitaani kwasababu wanaelewa vyema, aliongezea.

Gen Tumwiine alisema kuwa kikosi hicho cha LDU kitahudumu kama maafisa wa ujasusi na kuimarisha juhudi za maafisa wa polisi kukabiliana na uhalifu.

Hatujaweka mbinu za kiteknolojia na tunaamini kwamba jicho la binaadamu ndio la kuaminiwa zaidi kwa sasa. tulifanikiwa katika siku za nyuma na tuna imani.

'Wanakodisha bunduki zao'

Hatahivyo baadhi ya wanaharakati wana hofu kuhusu uanzishwaji wa kikosi hicho wakisema kuwa serikali ilikuwa imeunda kikosi hicho hicho miaka kumi iliopita lakini kikaosa heshima.

Wanachama wake walidaiwa kuwapatia wahalafu bunduki zao mbali na kubadilika na kutumia vifaa vyao kutekeleza uhalifu kama ilivyoripotiwa na gazeti la serikali la New Visoion mara kwa mara wakati huo.

Walikuwa hawana mazingira mazuri ya kufanya kazi hivyobasi wakawa miongoni mwa matatizo badala ya suluhu.

watu walipiga foleni

Chanzo cha picha, Allan Atulinda

Maelezo ya picha, Maelfu walituma maombi wakiwa na matumaini ya kupata ajira