Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Miili ya watu zaidi ya 40 yaripotiwa kuopolewa Mwanza, Tanzania
Miili ya watu 44 imeopolewa kutoka Ziwa Victoria baada ya kivuko kilichokuwa kimebeba mamia ya abiria kuzama jijini Mwanza Kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Ukerewe,Kanali Lucas Magembe amesema waliokolewa wakiwa salama ni watu 37, watu 32 wako hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Juhudi za uokoaji ziliendelea mpaka majira ya saa mbili usiku ambapo zoezi hilo lilisitishwa kutokana na hali ya giza ambayo ilikuwa kikwazo kutekeleza zoezi hilo.
''Sababu nyingine ni kuwa nguvu kubwa inahitajika na inahitaji ushiriki wa jamii na watu wengi walikuwa wameshachoka, hasa wale wenye mitumbwi ambao walikuwa wakifika pale kubeba miili'' alieleza Kanali Magembe.
Taarifa za awali zinaeleza kwamba kivuko hicho kilikuwa kimebeba mamia ya abiria.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima ameeleza kwamba maafisa kadhaa kutoka eneo hilo wakiwemo polisi na jeshi la majini wanaelekea kujiunga katika jitihada za uokoaji.
''Hatuijui hali halisi tunakwenda kuikagua kwanza halafu baadaye tutatoa tamko rasmi.
Malima ameeleza kwamba maboti ya polisi na jeshi yatashirikiana katika zoezi hilo.
''Tunaomba mungu atupe subira kwa wakati huu, na tusishuhudie idadi kubwa ya vifo'
Mkasa huo umewashutusha wengi nchini kama mwanamke mmoja aliyeshuhudia mkasa huo ambaye alionekana kujawa na hisia.
''Tazama Tazama.. Kivuko kile pale kimezama …….miili inaelea, imezama sasa hivi''.
Mikasa ya vivuko kuzama Tanzania
Tanzania ina historia ya ajali za vivuko kuzama, kibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kilikuwa mnamo Mei 1996, wakati MV Bukoba ilipozama kutoka Mwanza katika ziwa lilo hilo Viktoria kaskazini magharibi mwa Tanzania na kusababisha vifo vya takriban watu 1000.
Rekodi rasmi hata hivyo iliopo ni watu 894 waliofariki.
Kumewahi kushuhudiwa pia mikasa mingine kama vile Mv Skagit kivukio kilichozama mnamo 2012 wakatikikiwa kimebeba abiria 290 wakiwemo watalaii 17 kutoka pwani ya Zanzibar.
Mwanza ni mji muhimu wenye bandari Tanzania katika ziwa Viktoria, inayopokea bidhaa kama pamba chai, kahawa zinazotoka magharibi mwa nchi hiyo.
Ziwa viktoria ni la pili kwa ukubwa duniani baada ya ziwa Superior Amerika kaskazini.