Sababu ya Afrika Kusini kuhalalisha utumizi wa bangi

Watu wakivuta bangi nje ya mahakama ya katiba nchini Afrika Kusini baada ya ukuzaji na uvutaji wa bangi kuhalalishwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watu wakivuta bangi nje ya mahakama ya katiba nchini Afrika Kusini baada ya ukuzaji na uvutaji wa bangi kuhalalishwa

Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika kusini imehalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kukuza kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi.

Wanaharakati wanaounga mkono utumiaji wa ban gi walisheherekea uamuzi huo wa kihistoria wakisema ''sasa tuko huru''.

Hata hiyyo itakuwa haramua kutumia bangi katika maeneo ya umma au kuiuza.

Baraza la ukuzaji bangi nchini Afrika Kusini limeunga mkono uamuzi wa mahahakama dhidi ya matumizi ya bangi na kutoa wito kwa serikali kuwaondolea mashtaka watu waliyopatikana na kileo hicho.

Uamuzi huu unamaanisha nini?

Uamuzi huu wa mahakama ni kumbusho kuwa katiba ya Afrika Kusini ni moja kati ya zile zenye uhuru mwingi duniani, inayounga mkono haki za watu na katika kesi hii, ni haki ya kukuza na kuvuta bangi faraghani, kinyume na matarajio ya serikali inayokumbwa na wasiwasi kuhusu athari kwa afya ya umma.

Uamuzi wa mahakama ya katiba unaangazia suala la haki ya mtu kufanya atakalo akiwa nyumbani kwake.

Athari kutokana na uamuzi huu ni kubwa na hazitabiriwi hasa kwenye mifumo ya sheria ya nchi, ambayo huwafunga maelfu ya watu hasa wale maskini kwa kutumia au kukuza kiwango kidogo cha bangi.

Kuna uwezekano kuwa kwa kuruhusu watu kukuza bangi yao nyumbani kutapunguza nguvu za magenge ya madawa ya kulevya miongoni mwa jamii nyingi.

Lakini polisi ambao wamapinga uamuzi huu watakuwa na wasi wasi kuwa uamuzi huo utaleta mchanganyiko na kutuma ujumbe usiofaa kwa magenge ya uhalifu.

About 100 Rastafarians and other members of the public sing and dance outside the Cape Town High Court in support of a court application to decriminalise dagga (marijuana/cannabis) on December 7, 2015 in the Cape Town centre.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Agizo hilo lilikuwa ushindi kwa wanaharakati wa bangi

Serikali haijaidhinisha kwa njia yoyote biashara ya bangi, ikimaanisha kuwa serikali haiwezi kunufaika kwa kutosa kodi sekta iliyo halali.

Mahakama iliipa bunge miezi 24 kubadilisha sheria hiyo kuambatana na agizo lake.

Watu wazima ambao watatumia bangi faraghani wanalindwa na agizo hilo hadi sheria hiyo ibadilishwe.

Mahakama haikueleza na kiwango gani cha bangi mtu anaweza kupanda kwa matumizi yake.

Bunge litaamua kuhusu hilo, amri hiyo ilisema.

Mwezi Aprili Zimbabwe ilikuwa nchi ya pili barani Afrika baada ya Lesotho kuhalalisha bangi kwa matumizi ya kiafya.

Je unazifahamu nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa?

Lesotho

Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo.Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho.

Wanaume wakijiandaa kuvuta bangi Afrika Kusini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanaume wakijiandaa kuvuta bangi Afrika Kusini

Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini.

Zimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi

Afrika Kusini

Afrika Kusini ni nchi ambayo ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuhalalisha bangi.Mwezi Aprili mwaka jana, ilihalalisha bangi kwa matumizi binafsi nyumbani, lakini haikuruhusiwa kuzalishwa au kuuzwa.

Tangu mwezi machi mwaka 2017, baada ya mahakama kuu ya Western Cape kuhalalisha matumizi ya bangi majumbani bado matumizi yake ni kinyume cha sheria, mpaka pale sheria itakapobadilishwa kuruhusu wafanyabiashara walime na kuwekeza kwenye kilimo cha bangi, vivyo hivyo kwa makampuni kutengeneza bidhaa zitokanazo na bangi na mawakala kusambaza bidhaa.

Katika kipindi cha miezi kadhaa nyuma, wale walioonyesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha bangi wameleta maendeleo makubwa kufungua milango katika uzalishaji wa bangi kwa ajili ya dawa.

Ghana

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Ghana ni mtumiaji wa tatu wa bangi duniani, asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 64 wanajihusisha na uvutaji wa bangi .

Zimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi

Kulikuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuhalalishwa kwa bangi, mjadala ambao uligonga mwamba wakati wa siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya.

Mamlaka nchini humo zinasema kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji chenye kilevi, na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatahimilika.

Pamoja na hayo Ghana inashirikiana na mataifa mengine ya Afrika Magharibi kuhakikisha kuwa wanapambana kukomesha matumizi ya bangi na usafirishaji katika ukanda wao.

Korea Kaskazini

Bangi hukua kwa wingi sana nchin Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni.

Wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume cha sheria.

Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta bila kificho.