Tume ya Ulaya yalenga kubuni ajira milioni 10 barani Afrika

Jean-Claude Juncker

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jean-Claude Juncker

Rais wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker amependekeza kuwepo kwa muungano mpya na Afrika, kuboresha uhusiano wa kiuchumi na pia kuongeza uwekezaji na ajira.

Kwenye hotuba yake ya kila mwaka Bw Juncker alisema mpango huo utasaidia kubuniwa mamilioni ya ajira barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano inayokuja.

Maoni ya Bw Juncker yanahusu kile anachokiita biashara huru kati ya mabara. "Suala hapa ni kuboresha mikatati iliyopo sasa ambayo inazipa karibu nchi zore za Afrika uwezo wa kufikia masoko ya Ulaya bila kodi."

Pendekezo hilo pia linawapa fursa zaidi watu kutoka afrika kuongeza maarifa kwa mfano kwa kusomea viuo vikuu vya Ulaya.

Director of Frontex, the European Border and Coast Guard Agency, Fabrice Leggeri, visiting one of its vessels in Spain in August 2018

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Walinzi wa mipaka na pwani za Ulaya

EU inapendekeza Jumla ya euro bilioni 40 katika kipindi cha miaka saba hadi mwaka 2021. "EU inataka kupanua uhusiano wake na Afrika ambayo ni sehemu muhimu sana duniani."

Pia Juncker alitangaza mipango ya EU kutuma walinzi wa mipaka 10,000 kukabiliana na uhamiaji haramu ifikapo mwaka 2020.

Hii ndiyo hotuba ya mwisho ya Bw Juncker kama rais wa Jumuiya ya Ulaya.

Frontex officer grabs a rope during an rescue mission off a Greek island in 2015

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mashirika ya Frontex na lile na ulinzi wa mipaka na pwani za Ulaya kwa sasa yamewaajiri watu 1,600

Mambo yaliyozungumziwa na Juncker...

Kuhusu usalama

Bw Jucker alisema EU inahitaji kuwa salama kutoka kwa vitisho vingi vinavyoikumbwa.

"Ni Ulaya dhabiti tu na yenye nguvu inayoweza kuwalinda watu wake kutokana vitisho vya nje na vya ndani - kutokana wa ugaidi na mabadiliko ya hali ya hewa."

Kuhusu uhamiaji

Mashirika ya Frontex na lile na ulinzi wa mipaka na pwani la Ulaya kwa sasa yamewajiri walinzi 1,600 kutoka Ulaya, kwa hivyo idadi mpya inayotajwa na Juncker ni ongezeko kubwa.

Bw Juncker zaidi alipendekeza kubuniwa shirika linahusika na kutoa hifadhi barani Ulaya amabalo litatoa msaada kwa nchi zinazowapa hifadhi watafuata hifadhi.

Alisisitiza hitaji la kuwepo njia halali za kuingia Ulaya. "tunahitaji wahamiaji wenye ujuzi," alisema.

Kuhusu Ugaidi

Kutakuwana sheria mpya za kutoa makala zinazohusuhu ugaidi kutoka kwa mitandao ndani ya saa moja.

Mitandao itahitajika kuwa na njia za kufuta kile kilicho kwenye mitandao laikini haijulikani ni mbinu gani zitatumiwa.

Pendekezo lililoandikwa linaamaanisha kuwa makampuni ambayo yashindwa kutimiza matakwa hayo yatakabiliwa na faini ya hadi asilimia 4 ya pato lao la mwaka mzima.

Kuhusu Uchumi

Uchumi wa ulaya umekuwa kwa mwaka mitano mfululizo, "hakujakuwa na idadi kubwa ya wanawake na wanaume milioni 239 kuwa kwenye ajira barani Ulaya," Bw Juncker alisema.

"Ukosefu wa ajira kwa vijana ni asilimia 14.8. Ni hali ya juu zaidi lakini pia ya chini zaidi tangu mwaka 2000."