Marekani yasitisha msaada kwa shirikal la misaada nchini Palestina Unrwa

Muda wa kusoma: Dakika 3

Marekani imeamua kusitisha ufadhili wake wote kwa shirika la Umoja wa Mataifa linalowasaidia wakimbizi nchini humo , kulingana na wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani.

Imelitaja shirika hilo la Unrwa kuwa lisilo halali.

''Utawala wa Marekani , ulichunguza swala hilo na kwamba imeamua kwamba halitoenedelea kutoa usaidizi wake kwa Unrwa'', msemaji wake Nauert alisema.

Msemaji wa Palestina rais Mahmoud Abbas amesema kuwa ni ''unyanyasaji'' dhidi ya watu wake.

''Adhabu kama hiyo haitabadili msimamo kwamba Marekani haina jukumu lolote katika eneo hili na kwamba haitaruhusiwa kutoa suluhu'', nabil Abu Rudeina aliambia chombo cha habari cha Reuters.

Amesema kuwa uamuzi huo ni ukiukaji wa maamuzi ya Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa Unrwa, Chris Gunness, alitetea shirikika hilo katika msururu wa machapisho ya twitter.

"Tunapinga kwa hali na mali ukosoaji kwamba shule za Unrwa, vituo vyake vya kiafya na msaada wake wa dharura sio halali'', aliandika.

Hatua hiyo ya hivi karibuni inajiri baada ya Marekani kutangaza mwezi Januari kwamba itazuia zaidi ya nusu ya ufadhili wake katika shirika hilo.

Je Unrwa ni nini?

Unrwa lilianzishwa kusimamia mamia ya maelfu wa raia wa Palestina walioachwa bila makao baada ya vita vya 1948 kati ya Waarabu na Waisraeli.

Shirika hilo linasema kuwa kwa sasa linasaidia zaidi ya raia milioni 5 wa Palestina mjini Gaza, West bank, Jordan, Syria na Lebanon, ikiwemo kutoa usaidizi wa kiafya, elimu na huduma za kijamii.

Marekani ndio mfadhili mkubwa wa Unrwa ambapo anatoa ufadhili wa $368m (£284m) mwaka 2016 na kufadhili asilimia 30 za oparesheni zake zote katika eneo hilo.

Utawala wa rais Trump ulikuwa umeahidi $60m kwa Unrwa mnamo mwezi Januari, lakini ukazuia ufadhili mwengine wa $65m.

Ufadhili uliosalia wa sasa unatarajiwa kufutiliwa mbali.

Kwa nini Marekani inashutumu Unrwa?

Marekani imetofautiana na Unrwa, na maafisa wa Palestina kuhusu maswala kadhaa.

Rais wa Marekani Donald Trump awali amekuwa akilalama kwamba Marekani haipati heshima kwa kiwango kikubwa cha fedha za usaidizi kinachotoa kwa eneo hilo.

Mapema mwaka huu, alitishia kukatiza ufadhili kwa Wapalestina kuhusu kile alichokitaja kukataa kuzungumza na Israel.

Marekani na Israel zimetofautiana na Unrwa kwamba Wapelestina ni wakimbizi walio na haki ya kurudi katika nyumba walizozitoroka wakati wa vita vya 1948 .

Nikki Haley, balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa , mapema wiki hii alisema kuwa Unrwa ilitia chumvi idadi ya wakimbizi wa Wapalestina waliohitajika kurekebishwa.

''Tunaangazia ukweli kwamba , ni kweli kuna idadi isiopungua ya wakimbizi ambao wanaendelea kupata msaada, lakini la muhimu, Wapalestina wanaendelea kuishutumu Marekani'', alisema.

Je Palestina inasemaje?

Siku ya Ijumaa, Balozi wa Palestina mjini Washington , Hossam Zomlot aliishutumu Marekani kwa kuunga mkono manane ya Israel kuhusu kila jambo ikiwemo haki za zaidi ya wakimbizi milioni tano wa Palestina.

''Marekani inaharibu sio tu hali ambayo tayari imeharibika lakini pia hatma ya amamni katika siku zoijazo'', aliambia AFP.

Je Israel ina maoni gani kuhusu hatua hiyo?

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hapo awali ametaka ufadhili wa Unrwa kupunguzwa polepole na majukumu yake kuchukuliwa na shirika la umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi UNCHR , ikidai kuwa Unrwa inachochea tatizo hilo la Wapalestina.

Hatahivyo alisema kuwa hatua yoyote itakayochukuliwa itakuwa na madhara yake.

Baadhi ya Waisraeli wameonyesha wasiwasi wao kwamba kudhoofisha kwa Unrwa kunaweza kuathiri uthabiti na kusababisha watu wenye itikadi kali katika eneo zima.

Je jamii ya kimataifa inasemaje?

Mapema siku ya Ijumaa , waziri wa maswala ya kigeni nchini Ujerumani Heiko Maas alisema kuwa taifa lake litaongeza mchango wake kwa shirika hilo kwa sababu mgogoro wake wa ufadhili unazua wasiwasi.

''Ukosefu wa shirika hili utazua hisia zisizoweza kudhibitika'', alisema bwana Maas.

Wakati huohuo katibu mkuu wa Umoja wa mataifa , Antonio Guterres, amesema kuwa ana matumaini na Unrwa na kuyataka mataifa mengine kusaidia kujaza pengo la msaada uliosalia.