Taliban: Watu 48 wakiwemo wanafunzi wauawa kwa bomu Afghanistan, Marekani yashutumu shambulio

Watu 48 wakufa na wengine 67 kujeruhiwa kutokana na bomu lililolipuka katika kituo kimoja cha masomo ya ziada mjini Kabul nchini.

Serikali ya Marekani imelaan tukio hilo.Tukio hili linarejesha nyuma harakati za kuleta amani ya kudumu ya taifa hilo.

Polisi wanasema kuwa mtu aliyekuwa amejifunga mabomu alifika katika kituo hicho cha elimu huko magharibi mwa Afghanstan na kujilipua kati kati ya wanafunzi waliokuwepo.

Kituo hicho cha elimu kipo katika eneo la Washia.Haijajulikana ni kundi gani limetekeleza mauaji haya,japo katika shambulizi la awali kundi wapiganaji wa IS lilikiri kuhusika katika shambulio liliwalenga watu Shia.

Msemaji wa Marekani Heather Nauert, anasema kuwa shambulizi hili ni moja ni moja ya hali ya kutaka kuoneza hofu.

'Serikali ya Marekani inalaani vikali na imeshitushwa sana na shambulio hili la kujitoa muhanga kwenye katika kituo cha mafunzo ya ziada ya elimu mjini Kabul. Tunatuma salaam za pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na tunawatakia wapone haraka wale ambao wanaendelea kupata matibabu kutokana na majeraha waliyoyapata.Na shambulio hili ni moja ya jitihada za kurejesha nyuma jitihada za watu wa Afghanstan kufikia hali ya Amani na usalama," Heather Nauert

Wengi kati ya waliojeruhiwa na bomu hilo ni vijana waliokuwa wakipata mafunzo ya ziada.Hata hivyo polisi 35 wameuawa pia wameuawa katika shambulio jingine kaskazini mwa Banglan.

Kundi la wapiganaji wa Talban limekanusha kuhusika na shambulio hilo,japo jamii ya waumini wa Kishia wamekuwa wakilengwa na Sunni.Shia wanaonekana kama wapaganani kutokana na tofauti za kidini zinazoibuliwa na Sunni.