Rais wa Venezuela Nicolás Maduro anasurika jaribio la kuuawa

Venezuelan President Nicolás Maduro (2nd left) during an outdoor event in Caracas. Photo: 4 August 2018

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Nicolás Maduro (wa pili kushoto)

Rais wa Venezula Nicolás Maduro anasema amenusurika jaribio la kumuua kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani iliyokuwa na vilipuzi.

Bwana Maduro alikuwa akizungumza wakati wa warsha moja ya kijeshi mjini Caracas wakati jaribio hilo la kumuua lilitokea.

Video ya hotuba yake inaonyesha rais akitazama juu ghafla kwa hofu huku wanajeshi kadhaa wakikimbia.

Bw Maduro ameilaumu Colombia kwa shambulizi hilo madai ambayo yakananushwa na Colombia.

Wanajeshi saba walijeruhiwa na watu kadhaa wakakamatwa kwa mujibu wa mamlaka za Venezuela.

Kipi kinafahamika kuhusu shambulizi hilo?

Kisa hicho kilitokea wakati Bw Maduro alikuwa akizungumza kwenye warsha ya kuadhimisha miaka 81 ya jeshi la taifa.

President Maduro (centre) and his wife Cilia Flores (left) react to a loud bang during the military event

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais Maduro (kati kati) nan mke wake Cilia Flores (kushoto) wakishtuka kutokana na mlipuko mkubwa

Ndege mbili zisizokuwa na rubani zilizokuwa zimejazwa milipuko zililipuka karibu na jukwaa la rais, kwa mujibu wa waziri wa mawasiliano Jorge Rodriguez

Bw Maduro baadaye alisema kuwa "kifaa kilichokuwa kinaruka kililipuka karibu na mimi, mlipuko mkubwa. Sekunde chache baadaye kulikuwa na mlipuko wa pili."

Picha kwenye mitandao wa kijamii zilionyesha walinzi wakimlinda Maduro wakitumia vifaa visivyopenya risasi baada ya shambulizi hilo.

Security forces check a building after explosions near the place where President Maduro was speaking. Photo: 4 August 2018

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Madirisha yaliyopasuka karibu na eneo Maduro alikuwa akizungumza

Bw Maduro aliilaumu nchi jirani ya Colombia na vikundi vingine vyenye uhusiano na Marekani kwa njama hiyo ya kutaka kumuua.

Aliongeza kuwa haka shaka kuwa rais wa Colombia Juan Manuel Santos alihusika na jaribio hilo.

Rais huyo wa Venezuela awali ameilaumu Marekani kwa kupanga kumuua lakini hajatoa ushahidi kuhusu hilo.

Serikali ya Colombia imekanusha kuhusika ikisema hakuna ushahidi kwa madai yake Maduro.

Armed soldiers stand guard in Caracas. Photo: 4 August 2018

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Wanajeshi wakilinda eneo shambulizi lilitokea