Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Google itawasilisha intaneti kwa vibofu Kenya
Mkusanyiko wa maputo makubwa hivi karibuni vitatumika kusambaza intaneti katika maenoe ya mashambani Kenya.
Kampuni mwenza ya Google - Loon imetangaza kushirikiana na kampuni ya mawasiliano Kenya Telkom kuwasilisha intaneti katika maeneo hayo.
Msafara huo wa vibofu vilivyo na antena za kuninginia vitapepea hewani katika anga ya baadhi ya maeneo ya nchi hiyo
Lakini wataalamu wanaonya kuwa huenda ushirikiano huo ukachangia kuwepo na upendeleo kwa kampuni hiyo katika sekta ya mawasiliano.
Mpango huo unajulikana kama Project Loon, teknolojia iliyotumika iliundwa na kitengo cha utafiti cha kampuni kuu Alphabet, X.
Makubaliano kamili hayajawekwa wazi.
"Tutashirikana pakubwa na Loon, kuwasilisha huduma ya kwanza ya inatenti ya kuzunguka, haraka iwezekanavyo, kwa kutumia vibofu vya intaneti vya Loon Africa," amesema Aldo Mareuse, mkurugenzi mtendaji wa Telkom.
Vibofu vya Loon vitapepea umbali wa 20km hewani kutoka ardhini, urefu ambao kampuni hiyo inasema ni kupita anga inayotumika kwa usafiri, na hata sehemu ambapo ndege hupepea.
kibofu hicho chenye ukubwa wa uwanja wa tenisi kimetengenezwa kwa polyethylene, na kujezwa hewa ya helium na kinatumia nishati ya juwa.
Vibofu hivyo vimeundwa kuweza kuelea hewani kwa miezi kadhaa kila moja na vitasogea kulingana na kasi na muelekeo wa upepo wa maeneo vinavyostahili kuwepo.
Kila kibofu kina antena inayotumika kutuma mawimbi ya intaneti inayotoka ardhini, na kusambaza huduma katika eneo lenye ukubwa wa kilomita mraba 5000.
Katika suala la ushirikiano huu mpya, Telkom Kenya itakuwa na jukumu la kutoa mawimbi ya intaneti, na Loon itaisambaza katika maeneo ya mashambani Kenya.