Kwa Picha: Kusalimiana kwa Donald Trump na Kim Jong Un na maana yake

Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un hatimaye wamesalimiana.

Lakini hakuna mtu alifahamu kile kingeendelea. Hapa tunachapisha picha kutoka mkutano huo kuonyesha kile kilichotokea.

Kwanza kabisa jukwaa lililo wazi

Worker vacuums spot where President Trump and Kim are expected to shake hands

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Maandalizi

Matayarisho ya mwisho mwisho yalifanywa kwa zulia jekundu kwenye hoteli ya Capella katika kisiwa cha Sentosa huku bendera za Korea Kaskazini na Marekani zikiwa nyuma. Ni nadra kuona bendera za Korea Kaskazini na Marekani zikiwa pamoja na ni ishara ya ushindi mkubwa kwa Kim kuonyesha kuwa nchi hizi mbili zimekuja pamoja zikiwa sawa.

Wote wanaingia jukwaani kutoka pande tofauti

US President Donald Trump (R) and North Korea"s leader Kim Jong Un (L) walk toward one another at the start of their historic US-North Korea summit, at the Capella Hotel on Sentosa island in Singapore on June 12, 2018.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wakiingia Jukwaani

Kama waliokuwa wamefanya mazoezi kuhusu hili, Trump aliingilia upande wa kulia huku Kim akiingilia upade wa kushoto

Kusalimiana kwa mikono kulidumu sekunde 12

Mr Trump and Mr Kim shake hands

Chanzo cha picha, AFP

"Nimefurahi kukutana nawe Bw Rais," ni maneno aliyoyatamka Bw Kim alipokutana na Bw Trump

Walisaliamiana kwa mkono kwa muda lakini muda walishikana mikono ulikuwa mfupi kuliko ule wa kawaida wa Trump.

U.S. President Donald Trump and North Korea"s leader Kim Jong Un meet at the Capella Hotel on the resort island of Sentosa, Singapore

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kisha Trump anaonekana akimwelekeza Kim

Kisha Trump anaonekana akimwelekeza Kim kutoka kwa zulia ishara kwamba alikuwa akidhibiti hali.

Mazungumzo

US President Donald Trump (R) and North Korea"s leader Kim Jong Un (L) sit down for their historic US-North Korea summit,

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wawili hao walionekana hao wakizungumza kabala ya kuelekea kwa mkutano wa ana kwa ana.

Wawili hao walionekana hao wakizungumza kabala ya kuelekea kwa mkutano wa ana kwa ana.

Wakati huo ulionekana wa kuchanganyikiwa kwa kuwa Kim alionekana akiangalia chini na Bw Trump akiweka pamoja mikono yake.

Akiongoza wakati wa kutembea

North Korea"s leader Kim Jong Un (L) walks with US President Donald Trump (R) at the start of their historic US-North Korea summit

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Trump na Kim wakitembea na Trump akiwa hatua mbele kidogo wakielekea kwa mkutano wa moja kwa moja uliodumu dakika 40.

Trump na Kim wakitembea na Trump akiwa hatua mbele kidogo wakielekea kwa mkutano wa moja kwa moja uliodumu dakika 40.

Kwa Trump sasa huenda akajipongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na shinikizo zake kwa Korea Kaskazini. Kwa Kim kuweza kukutana na kufanya mazunguznoa na Rais wa Marekani ni ushindi mkubwa.

Siku ya kusalimiana wa mikono mara nyingi

US President Donald J. Trump (R) and North Korean leader Kim Jong-un (L) shake hands across the table during the expanded bilateral meeting

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wote wakati wa kumalizika kwa mazungmzo ya pamoja na wakati walitoa taarifa ya pamoja kwa waandishi wa habari walisalimiana mara kadhaa.

Wote wakati wa kumalizika kwa mazungmzo ya pamoja na wakati walitoa taarifa ya pamoja kwa waandishi wa habari walisalimiana mara kadhaa.

Ikiwa ni kama ishara ya uhusiano na mambo mazuri bila ya kutojulikana wazi ni kipi walikubaliana.