Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanamume aliyeandamwa na nguruwe awaita polisi Marekani
Maafisa wa polisi hupokea simu zisizo za kawaida za watu wakiomba usaidizi, lakini kisa kimoja jimbo la Ohio kimewashangaza wengi. Polisi walipigiwa simu mapema Jumamosi na mwanamume aliyekuwa anahangaishwa na nguruwe.
Polisi walidhai pengine mwanamume huyo alikuwa anaota au alikuwa amelewa alipowaambia kwamba alikuwa anaandamwa na nguruwe akienda nyumbani.
"Tulifika kwa mwanamume huyo tuliyedhani alikuwa mlevi na kwamba alikuwa anaelekea nyumbani kutoka kwenye baa saa 11:26 asubuhi," polisi hao wanasema kwneye Facebook.
Lakini walipofika walimpata mwanamume alikuwa hajalewa hata kidogo, lakini hakufurahia kabisa kufuatwa na nguruwe.
Alikuwa anafutwa na nguruwe lakini hakujua afanye nini, polisi wa kituo cha Ridgeville Kaskazini wamesema.
Polisi mmoja alifanikiwa kumkamata nguruwe huyo na kumuingiza kwenye gari la polisi na kumpiga picha.
Nguruwe huyo pia alipelekwa kwenye seli (chumba cha kuwafugia mbwa wa polisi) kabla ya kukabidhiwa kwa mmiliki wake Jumapili asubuhi.