Afrika wiki hii Kwa Picha: Aprili 27 hadi Mei 3 2018

Sehemu ya picha nzuri kote barani Afrika na waafrika kwingineko duniani wiki hii

Nchini Kenya, watumbuizaji wakiwafurahisha raia waliojitokeza kwa sherehe za siku kuu ya Leba ya Mei 1 2018, Jijini Nairobi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Siku ambayo, wasanii wa kitamaduni wakitumbuiza raia katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi
Wanachama wa kikosi cha Ulinzi cha Sudan, wakisimama imara kumsubiri Waziri mkuu wa Ethiopia kuwasili Mjini Khartoum mnamo Mei 2 mwaka 2018

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wanachama wa kikosi cha Ulinzi cha Sudan, wakisimama imara kumsubiri Waziri mkuu wa Ethiopia kuwasili Mjini Khartoum
Mwanamke akitengeza nyungu ya udongo, wakati wa sherehe za ufunguzi wa siku ya utalii katika mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan mnamo Aprili 27, 2018

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mwanamke akitengeza nyungu ya udongo, wakati wa sherehe za ufunguzi wa siku ya utalii katika mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan.

Nchini Zimbabwe, kundi la mchezo wa kwata likitumbuiza raia wakati wa sherehe za kila mwaka za kimataifa za sanaa (Haifa) katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare

Ni Mei 1 , 2018, Nchini Zimbabwe, kundi moja la mchezo wa kwata likitumbuiza raia wakati wa sherehe za kila mwaka za kimataifa za sanaa (Haifa) katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Nchini Zimbabwe, kundi moja la mchezo wa kwata likitumbuiza raia wakati wa sherehe za kila mwaka za kimataifa za sanaa (Haifa) katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.
Nchini Zimbabwe, kundi la wasanii wakiwafurahisha wahusika katika kongamano la kimataifa la sanaa maarufu kama Haifa, mjini Harare, Mei Mosi, 2018

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Sherehe za kila mwaka zikionyesha kipawa maridhawa cha wanasaa wa nchi hiyo, eneo la ukanda wa Kusini mwa Bara Afrika, Uchezaji dansi, Muziki, maonyesho ya mavazi na usanii wa sanaa.
"Mabango" kujiburudisha na kujifurahisha kwenye fremu kubwa za picha, zilizotumika kupigia picha za kibinafsi ya rununu (Selfie), wakati wa sherehe za kila mwaka za Afrikaburn, zilizofanyika eneo la Tankwa Karoo, Calvinia, Afrika Kusini, Tarehe 27 Aprili 2018

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, "Mabango" kujiburudisha na kujifurahisha kwenye fremu kubwa za picha, zilizotumika kupigia picha za kibinafsi ya rununu (Selfie), wakati wa sherehe za kila mwaka za Afrikaburn, zilizofanyika eneo la Tankwa Karoo, Calvinia, Afrika Kusini.
Aprili 28, mwaka 2018 Rais wa zamani Malawi Joyce Banda, apigwa picha katik, katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Chileka, mjini Blantyre, baada ya kurejea nyumbani kutoka uhamishoni.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais wa zamani Malawi Joyce Banda, apigwa picha katik, katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Chileka, mjini Blantyre, baada ya kurejea nyumbani kutoka uhamishoni.
Askari wa kikosi cha 21 cha Motorized Infantry, akijiadaa kutoka katika doria ya usiku viungani mwa mji wa Buea, katika eneo linaloshuhudia uhasama na mizozo, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo mnamo Aprili 26, 2018

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Macho makavu ya askari wa Cameroon, wanapojiadaa kutoka katika doria ya usiku viungani mwa mji wa Buea, katika eneo linaloshuhudia uhasama na mizozo, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo....
Wanajeshi wa kikosi cha 21 cha Motorized Infantry, katika barabara za mji wa Buea, Kusini- Magharibi mwa Cameroon mnamo Aprili 26, 2018. Vuguvugu hilo lililoanza Novemba 2016, limesababisha mapigano ya silaha tangu Oktoba mwaka 2017

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wanajeshi wanaopambana na makundi madogo madogo ya wanaharakati wanaoshinikiza upatikanaji wa uhuru wa watu wanaozungumza lugha ya kiingereza- katika eneo moja linalopakana na Cameroon na Nigeria.
Mtu mmoja wa kiume raia wa Tunisia, akiliendesha baiskeli akipita mchoro wa Baiskeli ukutani kisiwani Djerba, kinachotembelewa sana na watalii, Mei 1, 2018

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Nchini Tunisia, mwanamume mmoja anendesha baiskeli kwa madaha, akipita mchoro wa Baiskeli ukutani katika kisiwa cha Djerba...
Aprili 30, 2018 mmojawepo wa waendesha Baiskeli nchini Morocco akiwaamkua wanawake na watoto anaposhiriki mbio za kilomita 600, katika maeneo ya milima milima ya jangwa la Titan.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mbio ya baiskeli ni haraka, lakini nchini Morocco, mwendesha baiskeli amechukua muda wake kuwapungia mkono wanawake na watoto anaposhiriki mbio za kilomita 600 kama Maili (372) , katika maeneo ya milima milima ya jangwa la Titan.
Mhudumu mwingine wa Hoteli akibeba jiko la mkaa wa mawe na mwengine mabomba ya maji ya mchanganyiko wa (shisha), kwenye mkahawa mmoja mjini Cairo, Misri, huku mchoro mkubwa ukionekana ukutani wa nyota wa soka ya kulipwa wa timu ya kandanda ya Liverpool, raia wa Misri, Mohamed Salah. Aprili 30 mwaka 2018

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mhudumu wa Hoteli akimpelekea mteja mabomba ya maji ya mchanganyiko wa (shisha), kwenye mkahawa mmoja mjini Cairo, Misri, huku mchoro mkubwa ukionekana ukutani wa nyota wa soka ya kulipwa wa timu ya kandanda ya Liverpool, raia wa Misri, Mohamed Salah.

Picha zote na AFP, Getty Images, Reuters na EPA