Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tillerson asitisha shughuli alizopanga kufanya Kenya leo baada ya kuugua
Waziri wa mambo nje wa Marekani, Rex Tillerson amesitisha shughuli alizokuwa anapaswa kufanya nchini Kenya kutokana na hali yake ya kiafya kutokuwa nzuri.
Hakuna ishara yeyote inayoainisha kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 anasumbuliwa na tatizo kubwa la kiafya.
Msemaji wake amesema,Tillerson amekuwa kwenye ratiba ngumu katika ziara yake ya Afrika wakati huo huo akitumia muda mwingi kwenye mazungumzo ya simu kufuatilia kazi nyingine nchini mwake kama vile suala la Korea Kaskazini.
Maasifa wamesema watahairisha baadhi ya ratiba ambazo bwana Tillerson alikuwa ameweka ikiwa ni pamoja na safari yake ya kwenda kuona eneo ambalo ubalozi wa Marekani ulikuwa umelipuliwa mwaka 1998.
Rex Tillerson amekuwa katika ziara ya mataifa matano ya Afrika tangu siku ya jumatano akiwa ameanzia Ethiopia na sasa yuko Kenya kwa siku ya pili.