Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nyoka mwenye sumu kali agunduliwa ndani ya mkebe wa chakula cha mtoto Australia
Mwanamke amegundua nyoka mwenye sumu kali ndani ya mkebe ambao mtoto wake anatumia kebeba chakula cha mchana nchini Australia.
Nyoka huyo aligunduliwa amejificha kwenye kifuniko wakati mama huyo alikuwa akiweka chakula kwenye mkebe huko Adelaide, kulingana mshikaji nyoka Rolly Burrel.
Bw Burrel alisema almshauri mwanamke huyo kufunika mkebe na kuupeleka nje wakati alimpigi simu kumuomba usaidizi.
Alimtaja nyoka huyo kama eastern brown, mmoja wa nyoka wenye sumu kali zaidi duniani.
He identified the reptile as an eastern brown, one of the world's most venomous snakes.
"Sio kitu ambacho ungetaka kukiona wakati ukiangalia kama mtoto wako kwa kweli alikula chakula chake," Bw Burrel aliandika kwenye Facebook.
Alisema nyoka huyo alitolewa salama.
"Ni bahati sana kuwa alimuona nyoka huyo kwa sababu mtoto hata hawezi kuhisi akiumwa na kitu kidogo," aliiambia BBC.
Mshikaji nyoka huyo alisema kuwa anashuku nyoka huyo aliiangia kwennye mkebe huo kwa sababu labda ndiko alipata giza.
Nyoka wa aina hiyo hupatikana maeneo ya pwani mwa Australia na amehudsika na vifo 23 tangu mwaka 2000 kwa mujibu wa utafiti.