Kwa Picha: Maisha baada ya janga la Ebola Afrika Magharibi
Imekuwa ni miaka minne tangu utokee mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola kwenye mataifa ya Magharibi mwa Afrika ya Liberia, Guinea na Sierra Leone. Mpiga picha Hugh Kinsella Cunningham amerudi kufuatilia jinsi watu wanavyoishi tangu ugonjwa huo uangamizwe

Chanzo cha picha, Hugh Kinsella Cunningham
Mlipuko huo wa mwaka 2014 ulisabisha vifo vingi zaidi kulika milipuko mingine yote ya ebola kwa jumla, tangu virusi vya ugonjwa huo vigunduliwe mwaka 1976.
Virusi hivyo viliathiri maeneo maskini kama West Point nchini Liberia.
West Pointi ni eneo lenye watu wengi huko Monrovia. Wakati serikali ilitangaza amri ya kutotembea na kulizingira eneo hilo kama njia ya kuzuia kusamba kwa ugonjwa huo ghasia zilizuka.

Chanzo cha picha, Hugh Kinsella Cunningham
Mjuu wake Eva Nah aliuawa na polisi wakati akiandamana kupinga hatua hiyo ya serikali. "Mama na baba yake walikufa kwa hivyo ni mimi nilikuwa nikimhudumia," alisema Eva.
Miaka kadhaa baadaye, fidia ya serikali kutokana na kuuliwa kwake imemwezesha Eva kuwasomesha watoto wengine kwenye familia.
Rita Carol alimpoteza dada yake. Alikuwa akiuza chakula kwenye barababara za West Point lakini ameweka akiba pesa za kutosha kuanza biashara yake.

Chanzo cha picha, Hugh Kinsella Cunningham

Chanzo cha picha, Hugh Kinsella Cunningham
Etta Roberts anafanya kazi kama muuguzi kwenye zahanati ya Kahweh, iliyo mashariki mwa Monrovia. Kawaida huwatibu wagonjwa 10 kwa siku kwa ugonjwa wa Malaria.
Mwanzilishi wa kliniki Reginald Kahweh, aligharamia jengo hilo baada ya kuwapoteza wazazi wake wote kwa ugonjwa wa Ebola. Kila mtu ni lazima ahakikishe kuwepo kwa jamii bora...eneo hilo limebuniwa kuwakumbuka wale waliokufa.

Chanzo cha picha, Hugh Kinsella Cunningham
Ugonjwa wa Ebola ulikuwa pigo kwa mfumo wa afya nchini Liberia ambapo uliilemea kwa haraka. Miundo msingi ya nchi hiyo ilikuwa tayari imeharibiwa na vita vya miaka 14 vya wenye kwa wenyewe na mifumo ya afya ilikuwa na wakati mgumu kutekeleza majukumu ya kawaida.

Chanzo cha picha, Hugh Kinsella Cunningham

Chanzo cha picha, Hugh Kinsella Cunningham
J Roberts anaishi enoe lililo karibu na bahari la West Point. Baada ya kumpoteza mke wake kwa ugonjwa wa Ebola alianzisha biashara. Mke wangu alichomwa badala ya kuzikwa kwa hivyo ninahisi kama alienda kabisa. Niliamua kuwalea watoto wetu wanne," anasema.

Chanzo cha picha, Hugh Kinsella Cunningham
Wafanyakazi wengi waliofanya kazi ya kuzika waathiriwa wa Ebola nchini Sierra Leone walikuwa ni masiki na walipata fursa hiyo kwa sababu hawakuwa na kazi.

Chanzo cha picha, Hugh Kinsella Cunningham

Chanzo cha picha, Hugh Kinsella Cunningham
Mohammed Kanu aliajiriwa na sarikali kuzika miili wakati wa Ebola, hajapata kazi nyingine na amebaki akitunza makaburi kwa mshahara kidogo.

Chanzo cha picha, Hugh Kinsella Cunningham
Picha zote haki miliki Hugh Kinsella Cunningham.












