Mashindano ya urembo wa ngamia Saudi Arabia yatumbukia katika kashfa

Chanzo cha picha, Reuters
Ngamia 12 wamepoteza sifa za mashindano ya urembo nchini Saudi Arabia baada ya wamiliki wao kuwachoma sindano ya kubadili maumbile.
Maelfu ya ngamia wameshirikiswa katika tamasha la Mfalme Abdulaziz na kushindanishwa kwa muonekano wa nyuso zao, nundu na maumbile yao.
Lakini majaji waliingia kati wakati walipogundua kwamba baadhi ya udanganyifu ulifanyika na baadhi ya wamiliki waliotaka kushinda tuzo za fedha.

Chanzo cha picha, Reuters
Vile vile tamasha hilo lina mashindano ya riadha ya ngamia na kuonja maziwa, lina tuzo ya fedha taslim dola milioni 57.
Mtandao wa habari wa The National imeripoti kuwa Ali Al Mazrouei, mwana wa mfugaji bingwa , alisema dawa ya botox ilitumika kwenye midomo, pua na hata taya.
"Dawa hiyo inavimbisha kichwa kwa hio ukimuona ngamia unadhani ana kichwa,mdomo na pua kubwa" aliezea Mazrouei.

Chanzo cha picha, Reuters
Majaji pia walikuwa wakishindanisha nundu na misuli ya ngamia.
Kabla ya tamasha hilo, vyombo vya habari vya Saudia viliripoti daktari wa wanyama alikamatwa akiwa pasua ngamia hao ili kuwabadilisha ukubwa wa masikio pamoja na kuwachoma sindano ya dawa ya kubadilisha maumbile.

Pia unaweza soma yafuatayo
Jaji mkuu Fawzan al-Madi amesema kuwa ngamia ni moja wapo wa "nembo ya Saudi Arabi"
Mashindano hayo ya urembo wa ngamia yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2000.













