Miungu ya Wahindi ina rangi gani?

Goddess Sita with her sons

Chanzo cha picha, Naresh Nil

Maelezo ya picha, Mmoja ya miungu ya Kihindu Sita akiwa pichani na watoto wake mapacha Luv na Kush

Nchini India ambapo ngozi nyeupe inasifiwa, vuguvugu jipya limeibuka na kuitazamia miungu ya Wahindi kuwa na rangi nyeusi zaidi.

Upendeleo wa ngozi nyuepe si kitu kipya nchini India na kwa miongo mingi, kuwa na ngozi nyeupe kunatafsiriwa kuwa bora zaidi.

Mafuta yanayochubua ngozi ni miongoni ya vipodozi vinavyouzwa zaidi nchini humo na waigizaji vinara wa kike na wa kiume wa Bollywood wanaonekana mara kwa mara kwenye matangazo ya vipodozi vinavyogeuza ngozi kuwa nyuepe zaidi.

Goddess Lakshmi

Chanzo cha picha, Naresh Nil

Maelezo ya picha, Mwanamitindo Suruthi Periyasamy alifurahi sana alipoitwa kumuigiza mungu wa utajiri Lakshmi

Miaka ya hivi karibuni, aina tofauti ya mafuta yamezinduliwa yanayodai kufanya nywele za kwapani kuwa nyeupe pamoja na sehemu za siri za wanawake, na matangazo yanawashawishi wateja kuamini kuwa muonekano wa ngozi nyeupe itasaidia kuboresha maisha yao kwa kupata kazi nzuri zaidi au kushinda mapenzi ya mtu wanaompenda.

Hivi karibuni,kumekuwa na kampeini kama "Dark is Beautiful" au Uweusi ni Urembo na "unfairandlovely" zinazotoa wito kwa watu kusherehekea ngozi nyeusi.

Maelezo ya video, Dawa za kuchubua ngozi zina madhara mwilini?

Hata hivyo upendeleo huo wa ngozi nyeupe bado umeendelea, na muongozaji wa filamu za matangazo, Bharadwaj Sundar anasema upendeleo huo hauishii kwenye viumbe vya ulimwengu bali upo pia kwenye viumbe wa mbinguni.

A calendar image of Hindu god Krishna with his consort Radha
Maelezo ya picha, Krishna, mmoja ya mungu anayetafsiriwa katika vitabu vya dini ya Kihindi kuwa na ngozi nyeusi naye pia anaoneshwa mara kwa mara akiwa na ngozi nyeupe

"Picha zote za miungu maarufu tunazozioana, picha katika kuta zetu nyumbani na sehemu za ibada, kwenye mabango madukani na makalenda yote yanaionesha ikiwa na ngozi nyeupe."

Bw Sundar anaelezea hata Krishna, mmoja ya mungu anayetafsiriwa katika vitabu vya dini ya Kihindi kuwa na ngozi nyeusi naye pia anaonesha mara kwa mara akiwa na ngozi nyeupe.

"Kila mtu hapa anapendelea uweupe. Lakini mimi nina ngozi nyeusi na rafiki zangu wote wana ngozi nyeusi pia. Kwa hivyo nitahisije ukaribu na miungu wenye ngozi nyeupe?"

Kujaza pengo hili, Bw Sundar anayeishi kwenye mji wa Chennai kusini mwa India, pamoja na mpigapicha walibuni "Dark is Divine" au Uweusi ni Ubora - mradi unaoonesha miungu ya kihindu kuwa na ngozi nyeusi.

Goddess Durga

Chanzo cha picha, Naresh Nil

Maelezo ya picha, Mungu kwa jina Durga

Waliwaleta wanamitindo wenye rangi ya ngozi nyeusi na kuwavalisha kama miungu na kuwapiga picha ndani ya siku mbili mwezi Disemba, matokeo yao ni ya kustaajibisha.

Tangu kampeini hio kuzinduliwa mwezi uliopita,Bw Sundar anasema amepokea simu nyingi and watu wamepokea kazi yake vizuri sana japo kuna baadhi ambao wamewashutumu kuwa na uonevu wakisema kuwa mungu Kali kwa muda mrefu amekuwa akioneshwa akiwa na ngozi nyeusi

Baby Krishna

Chanzo cha picha, Naresh Nil

Maelezo ya picha, Mtoto Krishna ni miongoni wa miungu maarufu katika dini ya Kihindu

Bw Sundar anasema yeye ni Mhindi aliyeshika dini na hakukusudia kutoheshimu mtu, lakini "tukiangalia kote, tunapata kwamba mara asilimia 99.99, miungu yetu ina ngozi nyeupe".

"Muonekano una sehemu kubwa katika namna ambavyo tunachukulia watu, hasa wanawake, tuliona ni jambo ambalo lazima tulizungumzie" ameelezea.

"Na kupitia mradi huu, tunajaribu kuikosoa imani ya kwamba weupe ni ubora kuliko weusi".