Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Saudi Arabia na Milki ya nchi za Kiarabu zaanza kutoza kodi kwa mara ya kwanza
Kodi ya bidhaa na huduma imeanza kutozwa kwa mara ya kwanza kabisa katika mataifa ya Saudi Arabia na Milki ya Nchi za Kiarabu.
Kodi hiyo ya asilimia tano itatozwa kwa bidhaa nyingi na huduma.
Mataifa ya Ghuba kwa miaka mingi yamewavutia wafanyakazi wa kigeni kwa ahadi kuwa hawatatozwa kodi.
Lakini serikali zinataka kuongeza kipato chao wakati bei za mafuata ziko chini.
Kodi hiyo ilianza kutekelezwa tarehe mosi Janauari mwaka huu katika nchi zote.
UAE inakadiria kuwa katika mwaka wa kwanza kipato kutoka kwa kodi kitakuwa dola bilioni 3.3.
Petroli, chakula, bili nyingine na vyumba vya hoteli sasa vitatoswa ushuru.
Mashirika yakiwemo la Fedha Duniani IMF kwa muda mrefu yamezitaka nchi na Ghuba kuacha kutegemea mafuta kwa pato lao.
Nchini Saudi Arabia asilimia 90 ya bajeti hutokana na mauzo ya mafuta huku UAE ikitegemea mafuta kwa asliimia 80.