Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wana wa ufalme wakamatwa Saudi Arabia
Mawaziri 11 miongoni mwao wakikwa wana wa ufalme wameachichwa kazi na hata kuzuiliwa katika Mabadiliko makubwa yaliyotangazwa kwenye serikali ya Saudia.
Wengine wanaozuiliwa ni mawaziri wa zamani ambao wamehusishwa na kashfa za rushwa.
Katika hatua hiyo ambayo si ya kawaida inaelekea mwana mrithi wa mfalme Mohammed Bin Salman ambaye ndiye anaesimamia kitengo cha kupambana na ufisadi, anapania kujitenga na kuwadhibiti wapinzani wake wenye mamlaka makubwa nchini humo.
Miongoni mwa wanazuiliwa ni wana wa wafalme mmojawao ni mtoto wa marehemu mfalme Abdullah Prince Miteb aliyekuwa mkuu wa kitengo cha kikosi cha kiusalama National guard ambapo sasa amepokonywa wadhfa huo.
Mwengine ni billionaire Prince Al-Waleed bin Talal.
Inaripotiwa kwamba hisa katika kampuni aliyoekeza huko uingereza iitwayo Kingdom Holding, zimeporomoka kutokana na hisia hizo.
Mwandishi wa BBC anaefuatilia kwa karibu swala hilo anasema mabadiliko hayo bila shaka yatawabugudhi wale wanaopendelea mambo yabaki yalivyo Saudia ambako wenye mamlaka ya juu ya kiukoo na kikabila hawapendelei hatua kama hizo za kubadili mambo gafla.