Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Shirika laomba radhi treni kuondoka sekunde 20 mapema
Shirika moja la reli Japan limeomba radhi baada ya moja ya treni zake kuondoka sekunde 20 mapema.
Wasimamizi wa shirika la treni za reli ya Tsukuba Express kutoka Tokyo hadi Tsukuba wanasema wameomba radhi sana kwa usumbufu ambao huenda waliwasababishia wasafiri.
Kupitia taarifa, shirika hilo limesema treni hiyo ilikuwa imepangiwa kuondoka saa 9.44.40 (Saa tatu na dakika arobaini na nne na sekunde arobaini na nne) lakini iliondoka saa 9.44.20.
Wengi wa watu mitandaoni, hasa kutoka mataifa mengine wameshangazwa sana na hatua ya shirika hilo.
Shirika hilo limesema kosa hilo lilitokana na hatua ya wafanyakazi wake kutoangalia vyema ratiba ya treni kabla ya kuondoka.
Wameongeza kwamba hakuna mteja yeyote aliyelalamika kutokana na hatua ya treni hiyo kuondoka mapema kutoka kituo cha Minami Nagareyama kaskazini mwa Tokyo.
Tsukuba Express huwasafirisha abiria kutoka Akihabara mashariki mwa Tokyo hadi Tsukuba kwa dakika 45.
Ni nadra sana kwa treni Japan, nchi iliyo ya mfumo wa treni wa kuaminika sana duniani, kuondoka wakati ambao haipangiwi kuondoka.
Reli ya Tokkaido, inayotoka Tokyo hadi Kobe, husafirisha watu karibu 150 milioni kila mwaka.