Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa Picha: Mafuriko yasababisha hasara Dar es Salaam
Mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha maeneo mengi pwani ya Tanzania imesababisha mafuriko na uharibifu mkubwa.
Katika eneo la Mji Mpya, Kawe, nyumba zimebomoka na baadhi ya maeneo hayapitiki.
Mwandishi wa BBC Eagan Salla ametembelea maeneo hayo na anasema nyumba zaidi ya 20 zimeharibiwa vibaya na mafuriko.
Hizi hapa ni baadhi ya picha za hali ilivyo mtaani humo.
Mmoja wa wakati aliamua kuanika nguo zake zilizoloa maji zikauke.