Benki inayodaiwa kuchangia mauaji wa kimbari Rwanda yafanyiwa uchunguzi

Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalizuka baada ya ndege iliyokuwa imembeba Rais Juvenal Habyarimana kutoka kabila la Hutu ilidunguliwa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalizuka baada ya ndege iliyokuwa imembeba Rais Juvenal Habyarimana kutoka kabila la Hutu ilidunguliwa

Ufaransa imeanzisha uchunguzi dhidi ya benki ya BNP Paribas, kufuatia madai kuwa ilihusika na mauaji kimbari nchi Rwanda mwaka 1994, ambapo zaidi ya watu 800,000 waliuawa.

Mashirika matatu ya umma yamepeleka kesi mahakamani dhdi ya benki hiyo, wakiilaumu kwa kupitisha dola milioni 1.3 kwa muuza silaha.

Pesa hizo zilitumiwa kununua silaha na kukiuka azimio la marufuku ya silaha la Umoja wa Mataifa.

Kanali wa kabila la Hutu ambaye alipokea silaha hizo, Theoneste Bagosora, anatumikia kifungo cha miaka 35 jela kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalizuka baada ya ndege iliyokuwa imembeba Rais Juvenal Habyarimana kutoka kabila la Hutu ilidunguliwa Aprili tarehe 6 mwaka 1994.

Wanamgambo wa Hutu kisha wakawaua watu wa Tutsi walio wachache katika kipindi cha siku 100.