Washindi watuzwa kombe la Charity ''Sheild'' kimakosa Tanzania

Chanzo cha picha, Twitter
Makosa ya herufi yanaweza kuwa ndoto mbaya kwa mwandishi yeyote yule.
Hatahivyo makosa hufanyika na binadamu yeyote yule na anapotambua makosa hayo yeye husahihisha.

Chanzo cha picha, Twitter
Lakini sio kama makosa ya herufi katika kombe kubwa la soka.
Siku ya Jumatano usiku klabu ya Simba iliwalaza wapinzani wao wa jadi Yanga kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya kombe la kufungua msimu la Community Shield.
Lakini ni mashabiki waangalifu walioona makosa ya herufi katika maandishi ya kombe hilo.
Neno Shield liliandikwa kimakosa na kusomeka ''Sheild'' lakini hilo halikusitisha sherehe za kulikabidhi kwa mshindi kombe hilo.

Chanzo cha picha, Twitter
Kulingana na gazeti moja nchini Tanzania, mamlaka ya soka nchini humo sasa imeomba msamaha kwa kosa hilo.








