Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Bunge la wawakilishi Marekani launga mkono vikwazo dhidi ya Urusi
Bunge la wawakilishi nchini Marekani limepiga kura kuweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi licha ya Rais Donald Trump kupinga.
Maafisa wa vyeo vya juu watalengwa kujibu madai kuwa Urusi iliingilia kati uchaguzi wa Marekani mwaka 2016.
Mswaada huo unatarajiwa kukwamisha juhudi za Trump za kuboresha uhusiano na Urusi.
Mswaada huo unatarajiwa kupitia kwa Seneti kabla ya kupelekwa kwa Rais ili kuwekwa sahihi.
Ikulu ya White House inasema kuwa inatathmini mswaada huo na haijulikani ikiwa Rais ataukataa.
Uhusiano kati ya Urusi na Rais Donald umeuandama kwa kipidi cha miezi sita ofisini kufuatia madai kuwa urusi iliingilia kati kumsaidia apate kuchaguliwa.
Trump naye amemuwekea shinikizo mwanasheria wake mkuu kufuatia uchunguzi huo unaohusu Urusi. Amemtaja hadahari Jeff Sessions kuwa mtu dhaifu na kusema kuwa alikasirishwa na hatua ya Sessions kujiondoa kutoka kwa uchunguzi huo.
Bunge la wawakishi lilipiga kura kwa wingi kuunga mkono hatua dhidi ya Urusi ambazo pia zitasababisha vikwazo zaidi kuwekwa dhidi ya Korea Kaskazini na Iran kufuatia majaribio yao ya makombora ya masafa marefu.