Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
UN: Ukanda wa Gaza haukaliki kwa wakazi milioni mbili
Umoja wa Mataifa umesema Ukanda wa Gaza haukaliki kwa wakazi wake wapatao milioni mbili.
Katika ripoti inayoangalia hali ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa umesema kiwango cha kipato, huduma ya afya, elimu, huduma ya umeme na maji safi ya kunywa imezorota katika kipindi cha miaka kumi tangu Hamas ichukue madaraka katika eneo hilo.
Baada ya kuchukua utawala, Israel ambayo inaitambua Hamas kama kundi la kigaidi, ikishirikiana na Misri wameitenga Gaza.
Mamlaka ya Palestina, ambayo inadhibiti eneo la West Bank imesitisha uhamishaji wa fedha katika ukanda huo wa pwani na kuitaka Israel kupunguza huduma ya umeme.