Qatar kudai fidia kutoka nchi zilizoitenga

Chanzo cha picha, Getty Images
Nchi ya Ghuba ya Qatar imesema itadai fidia dhidi ya nchi zake jirani zilizoitenga nchi hiyo hasa kiuchumi.
Nchi za Saudi Arabia, UAE, Bahrain na Misri zote zimekata mahusiano ya anga, ardhi na bahari na Qatar baada ya kuishutumu kuunga mkono makundi ya kigaidi.
Qatar imekana madai hayo, na imeunda tume itakayoshughulikia malalamiko ya hasara iliyopatikana kwa kampuni zake pamoja na watu binafsi.
Walalamikaji hao wanaweza kuwemo shirika la ndege la taifa, ambalo limebidi kubadili njia licha ya awali kutumia anga za nchi jirani.

Chanzo cha picha, Empics








