Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rais Macron ataka kukomesha ugaidi
Rais wa Mali Emmanuel Macron ameelezea dhamira yake ya kusaidia kukomesha vitendo vya kigaidi na mauaji katika ukanda wa Sahel, Afrika Kaskazini.
Alikuwa akizungumza katika mkutano wa masuala ya Usalama nchini Mali uliohudhuriwa pia na viongozi kutoka nchi tano za eneo hilo, Mali, Mauritania, Niger, Burkina Faso na Chad.
Viongozi hao kwa pamoja wametaka kuungwa mkono, kwa kikosi cha wanajeshi elfu tano wanaopambana na wapiganaji wenye itikadi kali katika ukanda huo wa Sahel.
Rais Macron amesema majaribio hayo ya kupambana na ugaidi yanahitaji juhudi za pamoja kuimarisha maendeleo katika kanda hiyo, ikiwemo mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia ya nchi na kuimarisha utawala bora.
Amesema kinga nzuri ya kupambana na wapiganaji wa itikadi kali ni kuungana kwa pamoja na uthabiti.
Ufaransa imepeleka wanajeshi kadhaa katika eneo hilo la Sahel, toka ilipoingilia kati mgogoro wa Mali miaka minne iliyopita kuweza kuwafurumusha wapiganaji hao wenye itikadi kali ambao wanamafungamano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda.