Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Zaidi ya wafungwa 900 watoroka gerezani DRC
Gavana wa jimbo la Kivu ya Kaskazini Julien Paluku amesema zaidi ya wafungwa 900 wametoroka baada ya kutokea shambulizi na kuvunja gereza moja huko Congo DRC.
Watu 11 wameuawa katika tukio hilo Kaskazini Mashariki mwa mji wa Beni.
Haijajulikana ni nani haswa aliyefanya shambulizi hilo.
Mwanaharakati mmoja anasema kwa makundi mengi yaliyojihami yanayojulikana kama Mai-Mai yanaendesha shughuli zao eneo hilo.
Siku ya Jumamosi wafungwa kadhaa walitoroshwa na mtu mmoja aliyekuwa na silaha.
Mwezi uliopita mamia ya wafungwa walitoroka katika jela moja kubwa mjini Kinshasa baada ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha kuvamia jela hiyo usiku wa manane.