Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ireland kupata waziri mkuu wa kwanza mpenzi wa jinsia moja
Leo Varadkar anatarajiwa kuwa waziri mkuu nchini Ireland baada ya kushinda uongozi kwa chama cha Fine Gael.
Varadkar mwenye umri wa miaka 38, atakuwa waziri mkuu wa kwanza mpenzi wa jinsia moja na pia waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi kuwaia kuongoza nchi hiyo.
Bwana Varadkar alimshinbda wazari wa makao Simon Ceveney kwa asilimia 60 ya kura kuongoza chama cha Fine Gael, ambacho ndicho chama kikubwa zaidi katika serikali ya umoja.
Atachukua mahala pa Enda Kenny kama kiongozi wa chama cha kati kulia wiki chache zinazokuja.
Alijulikana kuwa mpenzi wa jinsia moja wakati wa kura ya maoni ya ndoa za jinsia moja mwaka 2015.