Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chanjo mpya dhidi ya virusi hatari vya rotavirusi yapatikana
Chanjo mpya dhidi ya maradhi hatari ya virusi vya rotavirus - yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya utotoni imethibitishwa kufaa na salama.
Upatikanaji wa chanjo hii umeonekana kama mafanikio makubwa pale itakapofika kwenye masoko kwa kuwa inatarajiwa kuuzwa kwa bei nafuu kuliko chanjo nyingine zilizopo na haihitaji kuwekwa ndani ya friji.
Matokeo ya majaribio ya chanjo hiyo yaliyofanyika nchini Niger yamechapishwa katika jarida la tiba la Uingereza.
Inakadiriwa kuwa watoto 1,300 hufa kila siku kutokana na kuhara kunakosababishwa na rotavirus.
Hadi sasa , chanjo mbili zimekuwa zikitumika kuzuwia maambukizi hayo, lakini zote ni ghali na lazima ziwekwe kwenye friji.
Watoto wengi katika jamii zenye kipato kidogo ambazo hazina huduma ya umeme hushindwa kupata chanjo hiyo.
Lakini sasa , shirika la madaktari wasio na mpaka - MSF -linasema kuwa chanjo mpya iliyofanyiwa majaribio nchini Niger inaweza kusaidia kuokoa maisha ya watoto wanaoihitaji zaidi.
Dawa hiyo mpya inaweza kutibu aina ya virusi vya rotavirus vinavyopatikana katika nchi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika.
Inatarajiwa kugharimu chini ya dola mbili unusu kwa kila mtoto.
Lakini kabla kutengenezwa ama kusambazwa chanjo zilizokuwepo kulihitaji kwanza idhini ya Shirika la Afya Duniani (WHO)