Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
DRC kuanza chanjo ya homa ya manjano
Leo serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kushirikiana na Shirika la Afya duniani WHO itaanza zoezi la kutoa chanjo ya homa ya manjano kwa raia wa nchi hiyo.
Jamuhuri ya Kidokrasia ya Congo na pamoja Angola ni miongoni mwa nchi barani Afrika zilizoathirika zaidi na ugonjwa huo.
Katika ripoti ya Shirika la Save the Children inaulezea ugonjwa huo ambao hauna tiba kama ugonjwa wa hatari unaoweza kusambaa zaidi duniani.
Hapo jana shirika hilo lilionya katika ripoti yake kuwa kama hatua hazitachuliwa ugonjwa huo unaweza kuenea katika mabara ya America, Asia, na Ulaya.