Wasichana 2 washambuliaji wa kujitolea mhanga wauawa Nigeria

Chanzo cha picha, AFP
Polisi nchini Nigeria wanasema kuwa wasichana wawili wanaokisiwa kuwa washambuliaji wa kujitoa mhanga, wameuawa kwa kupigwa risasi wakati walijaribu kuingia kaskazini mashariki mwa mji wa Maiduguri saa za usiku.
Polisi walisema kuwa kikosi cha kupambana na wanamgambo wa jihad kiliwafyatulia risasi wasichana hao wenye umri wa miaka 18 kabla ya kulipua milipuko yao.
Milipuko hiyo kisha iliharibiwa kwa nji salama.
Kundi la Boko Haram ambalo lilianzia mjini Maiduguri, limekuwa likiwatumia wanawake kama washambuliaji wa kujitoa mhanga.

Chanzo cha picha, AFP








