Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Iran yatimua meli ya Marekani
Meli ya jeshi la wanamaji wa Marekani ililazimika kubadili mkondo wakati chombo cha Iran kilichokuwa kikielea kwa mwendo wa kasi kilipoikaribia eneo la Hormuzi.
Meli hiyo ya USNS Invincible, ilibadili mkondo wakati chombo hicho cha Iran kiliikaribia umbali wa mita 550 kabla ya kusimama.
Meli zingine tatu za jeshi la Uingereza zilizokuwa zikiandamana na Meli hiyo ya Marekani wakati huo, nazo zililazimika kubadili mkondo.
Afisa moja wa Marekani alisema kuwa chombo hicho cha Iran kijaribu kuingia kati kati mwa meli hizo.
Afisa mmoja wa jeshi la Mareknai ambaye hakutaka kutajwa jina aliliambia shirika la AP kuwa visa kama hivyo vimekuwa vikitokea.
Jeshi la wanamaji wa Marekani linataja visa kama hivyo kuwa hatari na lilifyatua risasi kama onyo wakati vilitokea visa vya awali.
Meli hiyo ya Invincible ina mitambo ya radar na vifaa vingine vya kisayansi.
Meli kama hizo hutumika kuchunguza urushaji wa makombora na kukusanya habari muhimu.