Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Marekani yakana kuilipa kikombozi Iran
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani John Kerry, amekanusha vikali madai kwamba Marekani ililipa kikombozi cha dola milioni moja kuwakomboa wafungwa wa taifa hilo waliozuiliwa nchini Iran.
Amesema malipo hayo yalikuwa ya kutatua mgogoro kuhusu mpango wa ununuzi wa bidhaa za kijeshi.
Wanasiasa wa chama cha Republican wameshambulia serikali kutokana na malipo hayo.
Malipo hayo yalitolewa wakati wa kutia saini mkataba wa kinyuklia, na ubadilishanaji wa wafungwa ambapo wafungwa wanne wa Marekani waliachiliwa.