Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
"Shetani" wa wanyama pori afungwa miaka 12 Tanzania
Mmoja wa wawindaji hatari zaidi wa wanyama pori barani Afrika ambye pia anafahamika kama "Shetani" amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela nchini Tanzania.
Boniface Matthew Maliango, ambaye amekwepa kukamatwa mara kadha alitiwa mbaroni mwezi Oktoba.
Mwandishi wa habari ambaye alikuwa akifuatilia kesi hiyo kwenye mji wa Dodoma, anasema kuwa muwindaji huyo hatari alipatikana na pembe 118 zenye thamani ya zaidi ya dola 860,000.
Alizungumziwa kwenye makala moja wa Netflix, yanayofahamika kama Ivory Game, yaliyotengenezwa na mcheza filamu Leonardo DiCaprio.