Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa Picha : Kuhifadhi turathi za kisiwani Zanzibar
Majumba yaliyoko pwani mwa Tanzania, kisiwa cha Zanzibar yanaangazia usanifu wa ujenzi wa waswahili.
Baada ya miaka mingi ya kutelekezwa , majumba mengi yameporomoka.
Kwa sasa, kundi dogo la mafundi wanajaribu kutumia mbinu na maarifa ya jadi kuhifadhi majumba hayo
Stone Town, eneo la kihistoria la mji mkuu wa Zanzibar, lilitajwa na shirika la umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni ,UNESCO kuwa la kihistoria mwaka 2000.
Hata hivyo ni eneo lililoatharika kutokana na ongezeko la watu , msongamano wa magari na hali ya hewa kwenye kisiwa hicho.
Utumiaji ya saruji, kwa ukarabati, badala ya mchanga wa kale uliochanganywa na chokaa, umeongezea kupungua kwa nyumba nyingi kama ya the palace of Mtoni
Wanafunzi wa Zanzibar, waliopata mafunzo ya useremala na uashi walianzisha mradi wa kujenga majumba hayo ya urithi, kwa lengo la kuhifadhi majengo
Omar Yussuf Abdalla , mwenye umri wa miaka 38 , amesema kuwa mafunzo haya yatanilipa mshahara na kusaidi maisha yangu.
''Itawanisaidia mimi kuwafundisha wenzangu mbinu za kuhifadhi tamaduni zetu na mlango wa Stone Town.''
Picha na Aurelie Marrier d'Unienville