Ushahidi wa zamani kuhusiana na maisha 'wapatikana'

Chanzo cha picha, M DODD
Wanasayansi wamebaini mabaki ya mifupa ya vitu vya kale vilivyokuwa vikiishi duniani.
Mabaki hayo yanawakilishwa na vipande, vifundo na mirija ya mawe ya Canada inayokisiwa kuwa na miaka bilioni 4.28.
Wakati huo haujawachana mbali na uvumbuzi wa sayari na miaka milioni kabla kukubalika kama ushahidi kwa vitu vingi vilivyoishi duniani zama za kale
Watafiti wameripoti uchunguzi huo katika jarida la mazingira.
Na hayo madai yote , kuhusiana na maisha ya kale, ijapokuwa utafiti huo una utata kundi hilo la wanasansi linaamini lina uwezo wa kujibu maswali ya aina yoyote.

Chanzo cha picha, DOMINIC PAPINEAU
Mathew Dodd , aliyechambua mabaki hayo katika chuo kikuu cha London, Uingereza, anadai utafiti huo una uwezo wa kutoa mwangaza kwa chimbuko la maisha ya binadamu yalipoanzia.
''Utafiti huo unatoa majibu kwa maswali mengi kuhusiana na binadamu , kama vile anakotoka binadamu na kwa nini yuko hapa?
Mabaki hayo yalikuwa yamefunikwa katika sakafu ya baharini , inayojumuisha mawe ya zamani ya volcano.












