Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kanisa takatifu la 'mwujiza wa Yesu' lafunguliwa Israel
Misa maalum imefanyika kufungua rasmi kanisa Katoliki Kaskazini mwa Israel ambalo liliteketezwa na Wayahudi wenye itikadi kali mwaka wa 2015.
Kanisa hilo lililoko eneo la Tabgha kando mwa ziwa la Galilee linaaminika na Wakristo kama eneo takatifu ambapo Yesu Kristo alifanya muujiza wa kuwalisha watu 5000 kwa mikate mitano na samaki wawili pekee.
Ukarabati wa kanisa hilo ulichukua miezi minane na kugharimu kima cha dola milioni moja.
Licha ya Wayahudi watatu wenye itikadi kali kupatikana na makosa ya kuchoma kanisa hilo hata hivyo hawakuhukumiwa.
Uvamizi huo uliharibu maktaba ya kanisa na jengo nzima.
Hata hivyo sakafu yake iliyotengenezwa karne ya tano ilinusurika uharibifu huo.