Ndege ya Urusi yawaua wanajeshi wa Uturuki Syria

Ndege hiyo iliwashambulia kimakosa wanajeshi wa Uturuki

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Ndege hiyo iliwashambulia kimakosa wanajeshi wa Uturuki

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameomba msamaha baada ya shambulizi la Urusi kuwaua kimakosa wanajeshi watatu wa Uturuki kaskazini mwa Syria.

Wanajeshi hao walikuwa wakiwasaidia waasi nchini Syria, wakati wa jitihada za kuuteka mji wa al-Bab kutoka kwa kundi la Islamic State.

Hii ni sehemu ya hatua kubwa inayofanywa na Uturuki kuwatimua Islamic State, mbali na mpaka wa kusini mwa Uturuki.

Urusi na Uturuki ambao wanaunga mkono pande pinzani wamekuwa wakiwapiga vita Islamic State hivi majuzi kwa mashambulizi ya ndege.

Urusi na Uturuki wamekuwa wakiwapiga vita Islamic State

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Urusi na Uturuki wamekuwa wakiwapiga vita Islamic State