Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Marekani: Idara ya haki yatetea marufuku ya Trump
Idara ya haki nchini Marekani imeitetea marufuku ya usafiri ya rais Donald Trump na kuitaka mahakama ya rufaa kuiruhus kwa usalama wa taifa.
Taarifa ya kurasa 15 ilidai kwamba ilikuwa ni hatua ya halali kwa rais Trump na sio kuwapiga marufuku Waislamu.
Agizo hilo la rais liliwazuia kwa muda wakimbizi wote na wageni kutoka mataifa saba ya Waislamu.
Kesi ya kuikubali ama kuikataa marufuku hiyo imepangwa kusikizwa siku ya Jumanne.
Ombi hilo liliwasilishwa katika mahakama ya rufaa ya San Francisco baada ya agizo hilo la Trump kusitishwa na jaji wa mahakama ya kijimbo mjini Washington.
Jaji huyo alisema kuwa marufuku hiyo ni kinyume na katiba na inadhuru maslahi ya taifa hilo.
Kufuatia uamuzi huo raia kutoka mataifa saba ya Waislamu ikiwemo Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen walio na Visa halali waliweza kusafiri kuelekea Marekani.