Rwanda yawafuta kazi polisi 200 wafisadi

Serikali ya Rwanda imewafuta kazi polisi 200 wanaolaumiwa kwa kushiriia ufisadi.

Taarifa za shirika la AP zinasema kuwa msemaji wa Polisi Theos Bagede, alisema kuwa hakutakawa na huruma kwa polisi wafisadi.

Kufutwa huku kulithibishwa kwenye mkutano wa mawaziri siku ya Ijumaa ulioongozwa na Rais Paul Kagame.

Rwanda umesifiwa na nchi watoa misaada kwa kuwachukulia hatua maafisa wafisadi, na ni nchi ya tatu yenye viwango vidogo zaidi vya ufisadi barani Afrika, kusini mwa jangwa la sahara, kwa mujibu wa shirika la Transparency International.