Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kiongozi wa upinzani DRC Etienne Tshisekedi afariki dunia
Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi, amefariki dunia mjini Brussels nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 84.
Tshisekedi alikwenda mjini Brussels mwishoni mwa mwezi jana kwa ajili ya matibabu.
Bwana Tshisekedi alikuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe waliokuwa mstari wa mbele kupigania demokrasia ya nchi yake.
Alisimama kidete katika utawala wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Rais Mobutu Sese Seko, ambae utawala wake ulidumu kwa miongo kadhaa kabla ya kupinduliwa.
Etienne Tshisekedi pia alikuwa mpinzani wa Rais Laurent Kabila, ambae aliingia madarakani mnamo mwaka 1997, na mwanae, Rais Joseph Kabila, ambae hivi sasa ndio anatawala nchi hiyo.