Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kauli za Trump na Umoja wa Ulaya
Kansela wa Ujerumani , Angela Merkel , amesema kwamba umoja wa ulaya ni jibu bora kabisa kwa maoni yaliyotolewa na Donald Trump.Rais mteule wa Marekani amewamwagia sifa waingereza waliopiga kura ya kutaka kujiondoa katika umoja huo, na kuongeza kwamba anaamini kwamba nchi zingine zitaunga mkono uamuzi huo.
Angela Merkel amesema kwamba Ulaya inapaswa kuendelea kutetea utambulisho wake mwenyewe, ikiwemo sera zenye uwezo wa kukabiliana na changamoto tarajiwa za karne ya ishirini na moja.
Naye makamu kansela, Sigmar Gabriel, amerejea kile alichoandika Trump katika mitandao ya kijamii na kusema kwamba nchi yake iko imara kabisa na madai aliyoyatoa kuruhusu wahamiaji zaidi ya milioni moja kuingia Ujerumani ni "janga na makosa".
Gabriel amesema kwamba ni maamuzi ya Marekani huko Mashariki ya kati yamesababisha mgogoro wa wahamiaji.