Watu kadha wafa kwenye ajali ya mashua Tanzania

Mashua hiyo ilikuwa safarini kuelekea kisiwa cha pemba

Chanzo cha picha, SMARTFISH

Maelezo ya picha, Mashua hiyo ilikuwa safarini kuelekea kisiwa cha pemba

Watu kadha wanahofiwa kuaga dunia baada ya mashua iliyokuwa safarini kutoka mji wa bandari wa Tanga ikielekea kisiwa cha Pemba kuzama Jumatatu usiku.

Kamanda polisi eneo la kaskazini mashariki, Benedict Wakulyamba, aliiambia BBC kuwa mashua hiyo ilikuwa imewabeba watu 50.

Mkuu huyo wa Polisi alisema kuwa watu tisa wameokolewa na miili 12 kupatikana.

Kilichosababisha kutokea ajali hiyo hakijathibitishwa lakini kamanda wa polisi anasema upepo mkalia huenda ulisababisha mashua hiyo kupoteza mwelekeo.