Mkosoaji wa China ateuliwa kuongoza bodi ya biashara US

Rais mteule Donald Trump amemteua mkoasoaji mkubwa wa taifa la China kuwa kiongozi wa bodi ya biashara

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais mteule Donald Trump amemteua mkoasoaji mkubwa wa taifa la China kuwa kiongozi wa bodi ya biashara

Rais mteule wa Marekani Donald Trump, amemtaja mkosoaji mkubwa wa biashara za Kichina Peter Navarro kuwa kiongozi mkuu wa baraza jipya la kibiashara katika Ikulu ya White House.

Peter Navarro, alizindua sera ngumu dhidi ya Beijing na akaandika kitabu kwa jina "Death by China: How America Lost its Manufacturing Base". Yani kifo cha China: namna Marekani ilipopoteza uwezo wake wa uundaji bidhaa"

Serikali ya mpito ya Doland Trump, imemsifu kwa uwezo wake wa kufufua uchumi, mbali na kukabiliana na uhaba wa kazi kwa Wamarekani.

Peter Navarro mkoasoaji mkubwa wa China

Chanzo cha picha, University of California,Irvine

Maelezo ya picha, Peter Navarro mkoasoaji mkubwa wa China

Bwana Trump pia, ameteua mwekezaji bilionea na msomi wa uchumi, Carl Icahn, kama mshauri mkuu wa mageuzi.

Bw Icahn, amesema kuwa biashara nchini Marekani, imelemazwa na masharti mengi yasio na maana.