China yarejesha chombo cha Marekani

Chombo cha USNS Bowditch kilikuwa kikifanya utafiti

Chanzo cha picha, US Navy

Maelezo ya picha, Chombo hicho kilikuwa kinatumiwa na maafisa wa meli ya USNS Bowditch kufanya utafiti

Marekani imethibitisha kwamba China imerejesha chombo cha baharini ambacho kilikuwa kimetwaliwa kutoka kwenye bahari ya South China Sea.

Kutwaliwa kwa chombo hicho kulikuwa kumetishia kuvuruga uhusiano kati ya Marekani na Uchina.

Chombo hicho ni cha kufanya utafiti baharini.

Maafisa wa Pentagon wanasema chombo hicho kisicho na nahodha kilisalimishwa kwa maafisa wa Marekani karibu na pahala ambapo kilitwaliwa, kilomita 92 kaskazini magharibi mwa Ghuba ya Subic.

Taarifa ya Marekani imesema maafisa wake wataendelea "kupaa, kuendesha vyombo vya baharini, na kuhudumu katika bahari ya South China Sea" maeneo yanayoruhusiwa na sheria za kimataifa.

Baada ya kutwaliwa kwa chombo hicho, Rais Mteule wa Marekani Donald Trump aliituhumu China kwa kutekeleza wizi.

Manuwari ya Marekani iliokamatwa na China

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Chombo cha Marekani kilichokamatwa na China (cha rangi ya manjano)

Baadaye, alipendekeza China waruhusiwe kukaa na chombo hicho.