Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mourinho: Maisha ya Manchester ni mkasa
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa maisha ya upweke katika klabu hiyo ni mkasa na ameanza kuchoka na waandishi waliopiga kambi nje ya hoteli anayoishi.
Mourinho mwenye umri wa miaka 53,amekuwa akiishi katika hoteli ya mji huo ya Lowry tangu alipoajiriwa kama mkufunzi wa United msimu uliopita,Lakini mkufunzi huyo anasema kuwa hawezi kutembea nje kwa sababu ya usumbufu wa wapiga picha.
''Nataka kuvuka daraja hili na kwenda katika mkahawa. Lakini siwezi,kwa hivyo sifurahii'',Mourinho aliambia chombo cha habari cha Sky Sport.
United imekuwa na mwanzo tofauti tangu Mourinho alipochukuwa uongozi wa timu hiyo.
Wako katika nafasi ya saba katika jedwali la ligi,pointi sita nyuma ya viongozi Manchester City,na walishindwa 4-0 na klabu ya zamani ya Mourinho Chelsea siku ya Jumapili.