Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Trump: Kashfa ya udhalilishaji wa wanawake ni njama
Mgombea urais wa chama cha Republican Marekani Donald Trump amewaambia wafuasi wake kuwa shutuma za kukashifu wanawake ni njama ya kumfanya ashindwe uchaguzi wa Marekani.
Katika mkusanyiko na wafuasi wake huko Florida Trump amekanusha kuwa tuhuma hizo ni uongo.
Ikiwa zimebaki siku chache kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo Trump anaonekana kushindwa dhidi ya mpinzani wake Hillary Clinton.
Mapema mke wa Rais bi Michelle Obama amemshambulia Trump na kusema kuwa kitendo cha Trump cha Udhalilishaji wa wanawake ni cha Kushangaza na kutisha.