Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchumi wa nchi za Afrika washuka hadi asimia 1.6
Ukuaji wa uchumia kwenye nchi zilizo kusini mwa jangawa la sahara unatajiwa kushuka hadi asilimia 1.6 mwaka huu kutoka asilimia 3 mwaka 2015.
Hata hivyo ukuaji utakuwa kwa asilimia 2.9 mwaka ujao kwa mujibu wa utafiti wa kila mwaka wa benki ya dunia ambao ulitolewa kwenye mji mkuu wa Ivory Coast Abidjan.
Pia uchumi wa mataiafa ya Afrika unatarajiwa kupanda kwa asilimia 3.6 mwaka 2018.
Huku mataifa mengi ya afrika yakishuhudia kushuka kwa uchumi, baadhi ya nchi zikiwemo Ethiopia, Rwanda na Tanzania zimeendelea kupata ukuaji wa kila mwaka kwa zaidi ya asilimia sita.
Mtaiafa yakiwemo Côte d'Ivoire na Senegal yametajwa kuwa bora zaidi.